Pamoja katika kupunguza miguu kifundo

Share on Facebook10Tweet about this on TwitterShare on Google+0Share on LinkedIn0Pin on Pinterest0Share on StumbleUpon0Share on Tumblr0Share on Reddit0Email this to someone

“Pamoja katika kupunguza miguu kifundo”

Katika kuhakikisha kila mtoto anayezaliwa akiwa na tatizo la mguu kifundo anafikishwa mapema katika kliniki zetu na kupata matibabu yatakayompelekea kupona mapema, kliniki zote zinazotoa matibabu haya chini ya taasisi ya miguu kifundo Tanzania “TCCO” zimejipanga kuyafikia maeneo yoote yaliyopo mbali na kliniki zetu .

Shughuli za uhamasishaji na utoaji elimu juu ya miguu kifundo hutolewa ili kuondoa imani potofu katika jamii, kwa kufanya hivi jamii hupata uelewa na hivyo huwa tayari kushirikiana na wataalamu wetu kwa kuwafichua watoto wote wanaokuwa wamefichwa ama pengine kwa kutokujua ni wapi huduma hutolewa.

Share on Facebook10Tweet about this on TwitterShare on Google+0Share on LinkedIn0Pin on Pinterest0Share on StumbleUpon0Share on Tumblr0Share on Reddit0Email this to someone

Leave a Reply