Shiriki kutokomeza mguu kifundo

Share on Facebook37Tweet about this on TwitterShare on Google+0Share on LinkedIn0Pin on Pinterest0Share on StumbleUpon0Share on Tumblr0Share on Reddit0Email this to someone

Katika kuweza kufikisha ujumbe katika jamii zetu hasa ambazo bado hazijawa na elimu juu ya matibabu haya tuna njia ambazo huzitumia kufikisha taarifa juu ya matibaabu haya na wapi yanapatikana.

Njia hizo ni pamoja na;

  • Kubandika vipeperushi.
  • Kutoa matangazo ya Radio na Televisheni.
  • Mikutano, hapa huwa tunatembelea maeneo yao.

 

Katika kutekeleza dhamira hio, katika mwezi wa kumi na mbili hadi wa kwanza clinic za Kahama hospital, Shirati- Mara na Usa River ziliweza kutembelea maeneo tofautitofauti kutoa elimu juu ya miguu kifundo, kuondoa hofu na fikra potofu katika jamii pia kuwapa taarifa rasmi juu ya upatikanaji wa matibabu ya mguu kifundo.

Lengo hasa ni kupata watoto ambao kwa namna moja au nyingine hufichwa au wazazi kwa kutojua kama miguu hii hutibiwa basi huwaacha watoto pasipo huduma yeyote.

Baada ya matabibu wetu  kudhuru maeneo hayo kutoa elimu juu ya tatizo hili tuliweza kupokea watoto wapya ambao wazazi wao waliweza kupata elimu juu ya miguu kifundo kupitia mikutano hiyo. 

Wito kwa jamii.

“Tushirikiane kutokomeza miguu kifundo, miguu kifundo inatibika”.

Share on Facebook37Tweet about this on TwitterShare on Google+0Share on LinkedIn0Pin on Pinterest0Share on StumbleUpon0Share on Tumblr0Share on Reddit0Email this to someone

Leave a Reply